Shirika la Mpango wa Chakula duniani (WFP) jana lilitoa onyo kwamba mafuriko makubwa yataongeza hali mbaya ya usalama wa chakula na kusababisha njaa zaidi.
Shirika hilo limesema kuwa, watu karibu milioni 3 wameathiriwa, na zaidi ya watu milioni 1.2 wamepoteza makazi yao, kutokana na mvua kubwa kunyesha katika eneo lililokumbwa na ukame mwaka mmoja uliopita.
Mwenyekiti wa WFP katika kanda ya Afrika Mashariki Michael Dunford amesema kwenye taarifa iliyotolewa mjini Nairobi kwamba, mafuriko makubwa yanaleta maafa na kuonyesha hali isiyotabirika inavyoendelea kuadhibu eneo hilo. Na kutokana na kutabiriwa kwa mvua kubwa zaidi, hali mbaya zaidi bado haijafika.
Wataalamu wanasema kuwa, mvua kubwa zinazosababishwa na El Nino zinatazamiwa kuendelea mpaka mwanzoni mwa mwaka 2024.