WHO ilionya hapo awali kwamba karibu watu 100,000 nchini Somalia wanakabiliwa na viwango vya janga la njaa kutokana na ukame mbaya zaidi kuwahi kukumba eneo hilo katika kipindi cha miaka 40.
Kulingana na utafiti huo uliotolewa Jumatatu, kati ya watu 18,100 na 34,200 wanaweza kufa kutokana na matokeo ya ukame nchini Somalia katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu.
Hali mbaya ya hewa iliweza kusababisha “vifo vingine” 43,000 mwaka jana ikilinganishwa na ukame wa 2017, unaongeza utafiti ambao unabainisha kuwa nusu ya waathirika ni watoto walio na umri ulio chini ya miaka mitano.
Misimu mitano mfululizo ya mvua iliyoambatana na uhaba mkubwa wa maji katika maeneo ya Kenya, Ethiopia na Somalia imeua mamilioni ya mifugo, kuharibu mazao na kuwalazimu zaidi ya watu milioni moja kuondoka makwao kwa kwenda kutafuta chakula na maji.
Wataalamu wa Tabia nchi wanatarajia msimu wa sita wa mvua pia kukosa maji, na hivyo kuongeza hofu ya janga la kibinadamu ambalo halijawahi kutokea katika ukanda huo, hasa nchini Somalia.
Nchi hii tayari ilikumbwa na baa la njaa mwaka 2011 ambalo liliua watu 260,000, zaidi ya nusu yao wakiwa watoto walio chini ya umri wa miaka sita, kwa sababu jumuiya ya kimataifa haikuchukua hatua za haraka vya kutosha, kulingana na Umoja wa Mataifa.
Mwaka 2017, zaidi ya watu milioni sita nchini Somalia, zaidi ya nusu yao wakiwa watoto, walihitaji msaada kutokana na ukame wa muda mrefu katika Afrika Mashariki. Lakini hatua za mapema za kibinadamu ziliepusha njaa mwaka huo.