Shirika la Afya Duniani WHO limesema hapo jana kuwa linaendelea na uchunguzi kuhusu mlipuko wa ugonjwa usiojulikana uliogundulika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Katika mkoa wa Panzi, ulioko zaidi ya kilomita 700 kutoka mji mkuu Kinshasa, maambukizi 406 yameripotiwa na vifo 31. Wizara ya Afya ya Kongo imeripoti vifo vya ziada vilivyotokea nje ya vituo vya afya ambavyo vinavyohitaji kuchunguzwa na kuthibitishwa
WHO imesema katika taarifa yake kuwa visa vingi vimevyoripotiwa miongoni mwa watoto, hasa wale walio chini ya umri wa miaka mitano, huku dalili za ugonjwa huo ambao hadi sasa haujajulikana ikiwa ni homa kali, mafua na matatizo ya kupumua.
Magonjwa kama malaria, nimonia, UVIKO19 na utapiamlo vinachukuliwa kama vichecheo vya ugonjwa huo.