Featured

Shirika la Afya Duniani limetoa hii Top Ten ya sababu zinazoongoza kwa vifo duniani

on

Shirika la Afya Duniani lilikusanya taarifa za sababu za vifo mwaka 2012 na kuzifananisha na sababu kubwa za vifo mwaka 2000. Magonjwa ya moyo yamekuwa ni sababu kubwa ya vifo duniani kwani vimesababisha vifo vya watu milioni 7.4 mwaka 2012. Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile shambulio la moyo, saratani na kisukari yamesababishwa 68 % ya vifo vyote duniani mwaka 2012, kutoka 60% mwaka 2000. 

Ikilinganishwa na mwaka 2000, vifo vinavyotokana na HIV vimepungua kidogo, kipindupindu sio tena miongoni mwa sababu tano za juu zinazoongoza kwa vifo kwani imepungua kutoka vifo milioni 2.2 mwaka 2000 hadi milioni 1.5 mwaka 2012 . Vifo vinavyotokana na kifua vimepungua kutoka milioni 1.3 hadi milioni 1, na kifua kikuu hakipo tena kwenye top ten ya sababu za vifo.

Top 10 ya sababu zinazoongoza kwa vifo duniani 

  1. Shambulio la moyo 13.2%
  2. Kiharusi 11.9%
  3. Pumu 5.6%
  4. Maambukizi ya njia ya hewa 5.5%
  5.  Saratani ya mapafu na njia ya hewa 2.9%
  6. Virusi vya Ukimwi 2.7%
  7. Ugonjwa wa kisukari 2.7%
  8. Ugonjwa kuhara (Kipindupindu) 2.7%
  9. Ajali za barabarani 2.2%
  10. Shinikizo la damu na magonjwa ya moyo 2%

who

 

POOR COUNTRY


Mabadiliko ya sababu za vifo katika nchi maskini:2000 vs 2012

ULIIKOSA HII YA SABABU YA WATU 180 KUFARIKI KWA SAA? ANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments