Duniani

Rais Obama kaandika haya kuhusu mtoto aliyekamatwa na saa wakidhani ni Bomu…

on

September 16 2015 nilikusogezea stori kuhusu ishu ya mtoto wa miaka 14, Ahmed Mohamed mwanafunzi wa  MacArthur High School iliyoko Irving, Texas Marekani kukamatwa na Polisi baada ya kwenda na saa ambayo Walimu waliifananisha na Bomu !!

Ahmed

Ahmed aliibuni saa hiyo yeye mwenyewe, lakini kutokana na muonekano wake Walimu walishtuka wakijua kaibuka na Bomu Shuleni, good news ni kwamba hiyo ishu imefika mpaka White House, Ikulu ya Rais Barack Obama Marekani.

Rais Obama ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter ujumbe wa kumkaribisha Ahmed ndani ya Ikulu ya White House, kaonekana kuvutiwa na kipaji cha huyu mtoto na mwaliko huo kautoa kama njia ya kufanya watoto wengi waipende Sayansi na kuwa wabunifu.

OBAMA

Stori ya huyu mtoto kukamatwa iligusa kwenye Vyombo Vikubwa vya Habari Duniani ikiwemo BBC, hapa kuna kipande cha video chenye stori hiyo pia kama hukuipata.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments