Ni Septemba 1, 2021 ambapo klabu ya Simba SC imekutana na waandishi wa habari kuhusu kuelezea jezi mpya za msimu wa 2021/22.
Sasa miongoni mwa waliopewa kipaza sauti kuzungumza ni msanii wa Bongo Fleva Whozu ambae anafunguka kuhusu wimbo maalum utakaotumiwa na klabu hiyo.
“Nimetengeneza wimbo utakuwa maalumu kwaajili ya mashabiki wa Simba SC nimefanya hivyo kutokana na mapenzi ya timu yangu ya Simba SC, nimefanya hivyo kutokana na Ubingwa wa timu yangu”- Whozu
“Kwahiyo ni faraja kufanya kitu kizuri au kutengeneza ama kufanya ubunifu ni ushindi pekee kinajitangaza, asilimia kubwa ya baadhi ya nyimbo za wenzetu uwa wanawekeza kwenye nyimbo za Singeli lakini kwa upande wangu nimechanganya vitu tofauti tofauti kidogo nimeweka Bolingo, Singeli,Bongo Fleva sikutaka kukaa kwenye upande mmoja”– Whozu
“Kwahiyo nikaona nifanye collabo na mcongo nafikiri wengi mnafahamu Donat Mwanza na ndipo nikawasiliana kwanza na Uongozi wangu kisha tukawasiliana nae tukamuomba kurudia wimbo wake lakini tuufanye kwa lugha ya Kiswahili, basi tukafanikisha na wimbo unaitwa Simba ni noma”- Whozu
“Nafikiri ni makubaliano ya uongozi wa Simba na uongozi wangu watakubaliana lini video ya wimbo huo utokea na ninavyoongeza sasa wimbo tayari umeshatoka katika platform zote na unaweza kuupata kote, kikubwa naipenda Simba mimi ni shabiki wa Simba kindakindaki”– Whozu
SAMATTA AONDOKA FENERBAHÇE NA KUJIUNGA NA ROYAL ANTWERP