Ad

Michezo

Wiki ya majonzi kwa Yanga, rekodi mbili za vunjwa ndani ya saa 48

on

Timu za Simba na Yanga nj watani wa jadi na ndio timu Kongwe nchini Tanzania lakini sasa uhasimu wao umehamia kwa timu zao za wanawake Yanga Princess na Simba Queens ambazo leo zimekutana.

Yanga Princess leo amecheza Simba Queens kwa mara ya sita katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania bara, Simba Queens ikaibuka kidedea kwa ushindi wa magoli 3-0.

Magoli yakofungwa na Mwanahamisi Omary dakika ya 30, Opah kwa penati dakika ya 43 na Joell Bukuru dakika ya 50, ushindi huo umeipandisha kileleni Simba Queens kwa kuwa na point 39 na Yanga Princess kubaki nafasi ya pili kwa point 38.

Ila cha kufahamu ni kuwa Yanga Princess walikuwa Unbeaten leo ndio wamepoteza kwa mara ya kwanza lakini Yanga SC nao wamepoteza kwa mara ya kwanza jana dhidi ya Coastal Union kwa kufungwa 2-1 Mkwakwani Tanga.

Kingine cha kufahamu ni kuwa Yanga Princess haijawahi kuifunga Simba Queens zaidi ya kutoka sare mara moja na kufungwa mara tano kati ya sita walizocheza, Yanga Princess imewahi kufunga Simba Queens magoli mawili tu katika michezo yote hiyo.

Soma na hizi

Tupia Comments