Wilaya ya Mvomero kwakushirikana na Hifadhi ya Taifa Mikumi wamepanga kuanzisha mkakati wa kuhakikisha wanatangaza fursa ya Uwekezaji katika maeneo yaliyoko jirani na Hifadhi kwakuweka vivutio vya kitalii ili kupunguza ongezeko la Wanyama waharibifu wa mazao na vifo vya binadamu.
Hayo yamezungumzwa hapo katika kikao Cha pamoja kilichofanyika katika Ofisi za Hifadhi ya Taifa Mikumi kikihusisha pande zote zote mbili kwa upande wa Wilaya Mvomero uliwakilishwa na Mh Mkuu wa Wilaya Judith Nguli,Kamati ya Usalama.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mh Yusuf Makunja ,Mkurugenzi Mtendaji na baadhi ya wataalamu wa Halmashauri na kwa upande wa Hifadhi uliwakilishwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi Ignace Gara na Afisa Mwandamizi wa Hifadhi Herman Baltazary, lengo kuu ni kuangalia namna sahihi ya kuweka mkakati wa kutangaza fursa ya Uwekezaji katika maeneo yaliyoko jirani na Hifadhi husasani katika Vijiji vya Doma na Maharaka kuwa fursa ya Uwekezaji kwa kuweka vivutio vya kitalii.
Akizingumza katika kikao hicho Mh Mkuu wa Wilaya amewashukuru Viongozi wa Hifadhi kwakuweza kuona fursa hiyo na kujumuika kwa pamoja kuandaa mpango mkakati huo na kushirikisha Uongozi wa Wilaya ili kuwa kitu kimoja kuandaa fursa hizo za uwekezaji katika maeneo hayo yanayopakana na Hifadhi kwa kwa kufanya hivyo kutaweza kuwanusuru wananchi wa maeneo hayo kuepukana na Wanyama waharibifu lakini pia kutawawezesha wananchi hap kukupatia kipato kwa kulima mazao Kama ufuta lakini pia kuwekeza katika shughuli za biashara na Utamaduni.
Mh Judith Nguli amewata Wananchi hao kujiandaa kikamilifu kuchangamkia fursa hiyo kwani kwa mpango uliopo Sasa eneo la Doma ndipo litakuwa lango kuu la kuingilia Hifadhi ya Taifa Mikumi mala baada ya Serikali kusaini makubaliano Kuweka geti la kisasa ambapo Ujenzi huo utaanza na shughuli zote zote za kibiashara zitahamia katika eneo hilo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mh Yusuf Makunja amesema kuwa mpango huo utaunufaisha Halmashauri kwa kiasi kikubwa kwanza kwa wananchi kuepukana usumbufu wawanyama waharibifu ambao wamekuwa kero kubwa kwa wananchi wa maeneo hayo kiasi kwamba wamekuwa wakisababisha hifi vifo vya wanananchi lakini pia imekuwa fursa ya wananchi hao Sasa kukupatia kipato kwa kulimaazap ya kibiashara Kama vile ufuta lakini kuwekeza katika shughuli za kibiashara Kama vile kujenga mahoteli na kufanya shughuli za kiutamaduni
Aidha Mwenyekiti huyo amewataka Wataalam kuchangamkia fursa hiyo haraka iwezekanavyo kwa kufanya tathmini ya kina na kuandaa mchoro utakaoonyesha namna gani watapanga kisasa jinsi ya kutangaza eneo hilo kwa kuweka vivutio vya kitalii na hivyo kuwezesha Halmashauri kupata mapato kutoka eneo hilo .
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri amesema yeye pamoja na timu yake wameyapokea maelekezo hayo na watayafanyia kazi haraka iwezekanavyo kwa kuandaa mpango kazi utakao onyesha namna gani shughuli zitakavyoendeshwa katika eneo hilo na kuuwadhiridha katika kamati husika ili shughuli nyingine ziweze kuendelea.
Kwa upande wake Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Hifadhi Ignace Gara amesema baada ya kilimo Cha muda mrefu kutoka kwa wananchi wa maeneo hayo wao Kama Hifadhi wameamua kuja na mpango huo kwakuhakikisha kwanza wanaitangaza Hifadhi hiyo ya Mikumi lakini pia wanawawezesha wananchi walioko jirani na maeneo hayo na Halmashauri kuweza kujipatia kipato.