Habari za Mastaa

Will Smith amuomba radhi mchekeshaji Chris Rock

on

Usiku wa kuamkia Jumatatu zilifanyika utoaji wa tuzo za Oscar katika ukumbi wa Dolby Theatre huko nchini Marekani.

Miongoni mwa stori zilizochukua vichwa vya habari ni baada ya Muigizaji Will Smith kunyanyuka katika kiti chake na kufika jukwaani na kumzaba kibao Mchekeshaji Chris Rock.

Kitendo hicho kilizuia gumzo mitandao wengi wamejadili tofauti kitendo hicho, sasa Will Smith kupitia ukurasa wake wa instagram amechapisha ujumbe wa kuomba radhi kwa tukio hilo.

Staa huyo ameomba radhi kwa kusema..“Ningependa mbele ya Umma kukuomba radhi Chris Rock, nilikuwa nje ya mstari na nilikosea. vitendo vyangu havikuwa dira au mfano wa Mwanaume ambaye natakuwa kuwa– Will Smith

Hakuna nafasi ya vurugu kwenye hii dunia ya upendo na ukarimu. Pia naomba radhi kwa Academy na watayarishaji wa show, wahudhuriaji wote na watazamaji.” aliandika Will Smith

Smith amemuomba msahamaha Rock moja kwa moja, akisema alivuka mpaka pia ameomba msamaha kwa Chuo na familia ya Williams “Ninajuta sana kwamba tabia yangu imetia doa safari ambayo imekuwa ya kupendeza kwetu sote”

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Will Smith (@willsmith)

Tupia Comments