Winga wa Real Madrid, Vinicius Junior ameitaja ligi kuu soka nchini Hispania La Liga kama ‘ligi ya watu wabaguzi wa rangi.kbaada ya post aliyandika kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kufanyiwa ubaguzi wa rangi na mashabiki wa Valencia.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 Ameandika hivyo baada ya kufanyiwa ubaguzi wa rangi na mashabiki wa Valencia kwenye mchezo wa Ligi kuu Hispania La liga uliochezwa jana usiku mchezo ambao ulimalizika kwa Madrid kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Mestalla katika La Liga ya Uhispania, kulingana na meneja wa klabu Carlo Ancelotti.
Mchezo huo ulianza kipindi cha pili, ambapo baada ya mchezo kusimama, dk ya 73 Shabiki ‘mmoja aliyekuwa kwenye viwanja mchezaji huyo alisikika akimwita Tumbili, tumbili’
Watangazaji wa TV ya La Liga walisema kulikuwa na tangazo uwanjani likiwataka mashabiki kutowatukana wachezaji au kutupa vitu uwanjani.
Baada ya tukio hilo kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti amesema mwamuzi alipaswa kusimamisha mchezo huo kutokana na vitendo hivyo vya ubaguzu dhidi ya Vini.
Haikuwa mara ya kwanza, wala ya pili, wala ya tatu. Ubaguzi wa rangi ni jambo la kawaida kwenye La Liga. Taifa zuri, ambalo lilinikaribisha na ninalipenda, lakini limekubali kusafirisha sura ya nchi ya kibaguzi duniani.” Ameandika Vinicius
“It was not the first time, nor the second, nor the third,” it said. “Racism is normal in La Liga. The competition thinks it’s normal, the Federation does too and the opponents encourage it. I’m so sorry. The championship that once belonged to Ronaldinho, Ronaldo, Cristiano and Messi today belongs to racists.
“A beautiful nation, which welcomed me and which I love, but which agreed to export the image of a racist country to the world. I’m sorry for the Spaniards who don’t agree, but today, in Brazil, Spain is known as a country of racists.
Ancelotti alizungumzia hali hiyo baada ya mchezo huo akisema, “Sitaki kuzungumzia soka leo… wakati uwanja mzima unamwita mchezaji ‘tumbili’ kuna kitu kibaya kinatokea kwenye ligi hii.”
Katika mahojiano tofauti na wanahabari, Ancelotti alipendekeza waamuzi wasitishe mechi katika visa vingine vya ubaguzi wa rangi kwenye ligi. Muitaliano huyo alisema, “Nimesikitika sana kwa sababu La Liga ni ligi yenye timu kubwa zenye mazingira mazuri. Hili lazima tuondokane nalo. Tupo 2023, ubaguzi wa rangi sio lazima uwepo… njia pekee ya mimi ni kuacha mchezo.”