Top Stories

Wizara ya Afya yatoa tamko juu ya Virusi vya Corona

on

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewatoa hofu Watanzania kuwa ugonjwa wa Homa ya mafua makali ya virusi vya Corona hujaingia nchini huku akitoa wito kwa Watanzania kuacha kufanya safari katika nchi ambazo zimeripotiwa kuwa na ugonjwa huo kama hakuna ulazima.

Waziri Ummy ametoa taarifa hiyo Dodoma ambapo amesema kuwa Tanzania ina ushirikiano mkubwa wa kibiashara na nchi ya China na nchi nyingine hivyo ni vyema mkawa na tahadhari ya kusafiri pasipokuwa na ulazima ili kupunguza uwezekano wa kupata maambukizi.

Serikali imeshafanya maandalizi ya kuweka kambi maalumu ya kujaribu wagonjwa hao ambayo ipo Kigamboni DSM pamoja na zitakua hospitali zote nchini kuwajengea eneo maalum washukiwa wa ugonjwa huo pindi wanapoona dalili ili kupunguza uwezekano wa kuambukiza wengine.

BREAKING: MAGUFULI AMTUMBUA LUGOLA “UNANITESA, ONDOKA HAPA SINA URAFIKI KAZINI”

Soma na hizi

Tupia Comments