By using this site, you agree to the Privacy Policy and Terms of Use.
Accept
Millard AyoMillard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2024 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: Wizara ya Madini yaagiza ukaguzi leseni za Madini Njombe
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Millard AyoMillard Ayo
Font ResizerAa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2024 MILLARD AYO. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Top Stories > Wizara ya Madini yaagiza ukaguzi leseni za Madini Njombe
Top Stories

Wizara ya Madini yaagiza ukaguzi leseni za Madini Njombe

Published May 14, 2021
Share
1 Min Read
SHARE

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila amemwagiza Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Njombe kufanya ukaguzi wa Leseni zote 245 za Uchimbaji Madini mkoani humo ili kujua maendeleo ya uendelezwaji wake.

Agizo hilo linafuatia ombi lililowasilishwa na wachimbaji wadogo wa Madini mkoa wa Njombe ambao wameiomba Wizara kuwapatia maeneo ya kuchimba kutokana na sehemu kubwa kushikiliwa na wawekezaji kwa kipindi kirefu pasipo kuyaendeleza.

“Nakuagiza RMO fanya uchambuzi wa Leseni zote kujua zina hali gani, ikiwa zinalipiwa, ni maendeleo gani  yamefanyika ili kuanzia hapo wizara ichukue hatua. Tunapotoa leseni tunataka watu waziendeleze na wachimbe siyo kuzifungia kabatini,’’ Prof. Msanjila.

Prof. Msanjila ameongeza kuwa, moja ya vipaumbele vya Serikali na kama alivyoeleza Waziri wa Madini katika Hotuba yake ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2021/22 ni pamoja na kuwaendeleza, kuwarasimisha na kuwapatia maeneo wachimbaji wadogo   ili wachimbe, hivyo, wizara itahakikisha inalifanyia kazi kwa karibu suala hilo.

Amefanunua kuwa, endapo mmliki wa leseni ana nia ya kuiuza leseni yake hakatazwi isipokuwa anapaswa kuiendeleza kwanza kabla ya kufanya maamuzi mengine.

“Ukitaka kuuza leseni lazima useme uliifanyia nini kabla ya kuiuza. Huu ndiyo utaratibu wa Sheria,’’ amesema.

TAGGED:TZA HABARI
Share This Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article Mahakama yapinga Rais Kenyatta kubadili katiba
Next Article Waziri Mkuu ashiriki swala ya Eid “udhurieni Baraza la Eid Rais anakuja” (+picha)
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Habari kubwa Magazetini Kenya leo December 15, 2024
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo December 15, 2024
TRA Iringa yawashukuru walipa kodi wake
TRA mkoa wa Iringa yazidi kudumisha mahusiano na wafanyabiashara
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US
© 2024 MILLARD AYO. All Rights Reserved. Designed by Ayo.

Lost your password?