Top Stories

Wizara ya Maliasili yasitisha tozo za Lodge, kambi Hifadhini

on

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.Damas Ndumbaro amesitisha tozo ya pango ya ardhi kwa lodge na kambi za huduma za kitalii katika Hifadhi za Taifa ( TANAPA) kwa kipindi cha muda wa miezi mitatu kwa lengo la kutoa ahueni kwa Wadau wanaotoa huduma hizo kukabiliana na athari za ugonjwa wa UVIKO 19 kwenye sekta ya Utalii nchini.

Dk. Ndumbaro ameyasema hayo hivi karibuni Jijini Arusha wakati alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Chama cha Wasafirishaji Watalii Tanzania ( TATO).

Amesema tozo hiyo mpya iliyoanza kwa mwaka huu mpya wa fedha itasitishwa hadi mwezi Septemba mwaka huu.

Amesema tozo hiyo itatoa ahueni kwa Wadau wa Utalii ambao wanamiliki loji na kambi za huduma za kitalii ili waendelea kutoa huduma katika kipindi hiki kigumu na cha badae kutokana na ugonjwa wa UVIKO 19 kuitikisa kwa kiasi kikubwa sekta ya utalii duniani ikiwemo Tanzania.

“Nimesikiliza maombi ya TATO kwa kuwa Serikali lazima ipate mapato na Wadau wa Utalii lazima wafanye biashara ili wapate faida ili waendelee kulipa kodi, Nimeamua kusitisha kodi hiyo ili waweze kuendelea kufanya biashara utalii hadi mwezi septemba baada ya hapo maamuzi mengine yatafanyika kulingana na hali itakavyokuwa,” Dk.Ndumbaro.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TATO, Wilbard Chambulo amemshukuru Waziri Ndumbaro kwa kusitisha tozo hiyo hali itakayowasaidia kuhimili katika kipindi kigumu wanachokipitia cha ugonjwa wa UVIKO 19 ambapo nchi nyingi duniani zimefunga mipaka yao

HUZUNI MKE NA MTOTO WA TB JOSHUA WAMWAGA MACHOZI WAKIAGA MWILI

Soma na hizi

Tupia Comments