Serikali kupitia Wizara ya Nishati imepokea wazo la mbunge wa jimbo la Tanga mjini la kuwaunganishia umeme wananchi na kulipa kidogo kidogo kupitia matumizi ya kila siku ili wananchi wasiokuwa na uwezo wa kulipa kwa mkupuo waunganishiwe umeme.
Ummy Mwalimu ametoa ushauri huo kwa serikali ikwa ni mara ya kwanza kusimama bungeni na kuuliza swali kwa serikali tangu uteuzi wake ulipotenguliwa mwezi Agosti 2024
Ummy amehoji serikali kwanini isiwaunganishie wananchi Umeme kwa mkopo ili walipe kidogo kupitia matumizi ya kila siku ya umeme.
“Kuhusu kuunganisha umeme na kulipia kidogo kidogo tumepokea wazo la Mheshimiwa mbunge tutaanza kulichakata kuona namna ya kulifanyiakazi kwasaababu huko nyuma TANESCO walijaribu kufanya hivyo baadae lakini marejesho hayakuwa mazuri tutachakana na kuona ambavyo tunaweza kulifanyiakazi ili wananchi waendelee kupata huduma” Judith Kapinga Naibu Waziri wa Nishati