Top Stories

Wizara yazindua onesho la mchango wa wanawake kwenye utalii

on

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amefungua Onesho la Mchango wa Wanawake katika Sekta ya Utalii nchini lililofanyika leo kwenye kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Alisema onesho hilo litaonesha shughuli mbalimbali zinazofanywa na mwanamke za kuhamasisha utalii.

“Onesho hili linaonesha jinsi wanawake wanavyojihusisha na shughuli za kiuchumi na utalii ili kuinua kipato kwa kuonesha bidhaa zinazozalishwa, ujenzi wa nyumba za asili, ususi wa vikapu, utengenezaji vyungu, mapambo ya shanga , mafuta ya mawese na nazi” amesisitiza Mhe. Masanja.

Soma na hizi

Tupia Comments