Habari za Mastaa

Kingine kilicho-trend leo ni hii picha ya Davido na Wizkid pamoja

on

Picha za Davido na Wizkid wakiwa pamoja sio picha zinazotokea au kupigwa kila siku, kumbuka wawili kuwa na beef ambapo mwaka mmoja uliopita Davido alinukuliwa akisema ‘Wizkid hanipendi… toka nimeanza kujulikana kimuziki nimekua nalinganishwa au kupambanishwa na Wizkid, kitu watu hawajui sikuwahi kuwa na tatizo nae na tulikua tunakutana backstage na night club na tulikua poa tu

Wizkid aliwahi kuhojiwa na mtangazaji huyuhuyu pia akasema Davido anamuonea wivu sababu ya mafaniko yake…. haya yooote yalipita na wawili hawa wakaja kupatana na sasa wako poa na hata waliahidi kutoa single pamoja.

Davido 2

Kwenye Interview ambayo Davido akiongelea kutokupatana kwake na Wizkid

Tukiachana na hayo ya beef kitambo, mpya ni hii baada ya Davido kufanya bonge la show weekend iliyopita huko Congo Brazaville kilichochukua headlines April 4 2016 ni picha ya pamoja ya Wizkid na Davido ambayo ilipostiwa na Davido wakiwa kwenye ndege binafsi na aliandikanimerejea Lagos na kaka yangu Wizkid’

Wizkid Davido

Davido 5

Post ya picha ya Wizkid na Davido kwenye Twitter imekuwa RETWEETED na watu wengi ambao ni zaidi ya 800 mpaka mara ya mwisho naitazama tofauti na post zake nyingine zilizotangulia.

Wizkid naye alipost picha hiyohiyo kwenye page yake ya Instagram na kuandika ‘kileleni… sisi pekee’ ambapo mashabiki wengi wameonekana kufurahishwa na watu hawa ambao walionekana kuwa na uhasama, mashabiki wengine wamelilia ifanyike kolabo yao.

Wizkid

ULIIKOSA VIDEO YA DAVIDO AKIONGELEA BEEF YAKE NA DIAMOND PLATNUMZ? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line yatiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments