Habari za Mastaa

Unafahamu kilichoandikwa kwenye mitandao ya kijamii Nigeria kuhusiana na msanii Wizkid? Kisome hapa.

on

Taarifa zilizoenea mitandao mbali mbali ya Nigeria saa chache zilizopita zinazungumzia tukio kutoka Kenya linalohusiana na kukamatwa kwa msanii wa Nigeria Wizkid ambaye alishikiliwa na na jeshi la Polisi nchini humo saa chache kabla ya kupanda ndege kurejea Nigeria.

Taarifa iliyoandikwa na Standard Digital Kenya imesema, Wizkid alikamatwa hotelini Nairobi Crown Plaza ambapo amekaa kwa takribani wiki moja baada ya kufanya onesho lake.

Kwa mujibu wa habari kutoka chanzo hicho, Wizkid alikamatwa kwa kosa la kuvuta bangi hotelini hapo na baada ya mzozo wa muda mrefu baina yake na mhudumu wa hoteli hiyo, mhudumu wa hoteli alitoa taarifa polisi ambao walimkamata na kumfikisha kituo cha Capital Hill ambapo alipigwa faini ya sh. 50,000 za Kenya kwa kosa hilo na baadaye kuachiwa huru.

Wizkid alikamatwa hotelini hapo siku ya jumamosi kwa kosa hilo, ambapo Victoria Kimani, msanii wa Kenya ambaye wamefanya kolabo hivi karibuni ametajwa kuhusika kumtoa Wizkid kutoka kituo cha Polisi.

Wiz & VickyNi halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments