Habari za Mastaa

“Wakazi simfahamu kwa sura wala sijui kazi yake hata moja” – Afande Sele

on

Mwanamuziki mkongwe wa Hip Hop Tanzania Afande Sele amesema kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM akidai kuwa hamjui msanii wa Hip Hop Wakazi baada ya msanii huyo kuwataja wasanii wanaoandika mashairi na kusema Afande Sele hayupo technically. 

Baada ya kauli hiyo ya Wakazi, Afande Sele aliitumia account yake ya Twitter akiandika kuwa hamjui Wakazi kabla ya leo May 3, 2017 kuirudia kauli hiyo kupitia 255 akisema:

“Naapa mbele za Mungu kwamba Wakazi simfahamu kwa sura na sijawahi kumuona. Kazi zake sijawahi kuzisikiliza, isipokuwa jana jioni mshikaji mmoja alinikumbusha na kusema alishawahi kuimba kama Mangwea. Kwa hiyo, alijivisha umangwea baada ya kufariki, ila sijui kazi yake hata moja.

“Kuna kipindi nilijitoa kwenye Group ambalo tulikuwa wote, kwa sababu anajifanya anajua kila kitu wakati hajui kitu chochote. Sasa sioni kama kuna tija yoyote ya yeye kuniona labda mimi nafanya nini maana ni mtu ambaye hata ukisema uitishe show Manzese, hakuna anayemjua. Mimi mwenyewe simjui.”Afande Sele.

VIDEO: Q Boy kuhusu Dancer wa Justin Bieber kuucheza wimbo wake

Soma na hizi

Tupia Comments