Habari za Mastaa

Kitu Jackline Wolper kaongea toka kajiunga na CCM… kazisoma comments zao

on

Ilijulikana mwigizaji wa movie za bongo Jackline Wolper alikua mfuasi wa chama cha CHADEMA ambapo alimpigia sana debe mgombea wake wa urais Edward Lowassa kwenye uchaguzi mkuu wa 2015.

Kilichomfanya Wolper a-trend kwenye mitandao ya kijamii July 23 2016 ni baada ya kuonekana kwenye mkutano mkuu wa chama cha kisiasa cha CCM Dodoma na kutangaza kujiunga na chama hicho akitokea CHADEMA.

Baada ya hapo wengi wametoa maoni yao kwenye mitandao ya kijamii kuhusu maamuzi ya Wolper na usidhani kwamba Wolper mwenyewe hajayasoma, kwa sababu anapita kila siku kwenye mitandao ya kijamii, hii ndio kauli ameitoa kwa wale waliomponda na kumuita Msaliti.

Kwenye Exclusive na AyoTV na millardayo.com amesema >>> ‘Sikuwahi kuwa na kadi yoyote ile ya UKAWA na sasa hivi nimeamua kuingia CCM na sijashawishiwa wala kuhongwa, hakuna mtu amenivuta shati kuingia CCM’

Nimefanya haya baada ya kuona kile kitu nilikua nakitaka kwenye nchi yangu Rais Magufuli anakifanya sasa hivi, kwanini niichukie CCM? naipenda CCM na CCM ndio nyumbani‘ – Jackline Wolper

UNATAKA KUMSIKILIZA JACKLINE WOLPER ZAIDI KUHUSU KUJIUNGA CCM? BONYEZA PLAY HAPA CHINI….

ULIIKOSA HII YA JACKLINE WOLPER NA HARMONIZE MAPENZI MOTOMOTO? BONYEZA PLAY HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments