Top Stories

BREAKING: Wema alipa faini ya MILIONI 2, Wakili wake azungumza

on

Leo July 20, 2018 Baada ya hukumu ya Muigizaji Wema Sepetu kutolewa katika Mahakama ya Kisutu DSM Wakili wa Muigizaji huyo, Albert Msando amezungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa kesi hiyo imechukua muda mrefu kwasababu ilihitaji ushahidi wa kuthibitishwa.

Hata hivyo Msando amesema ni ukweli usiopingika kuwa Tanzania kuna tatizo la wasanii kutumia dawa za kulevya hivyo sasa Wema atakuwa Balozi mzuri kueleza madhara ya dawa za kulevya.

“Sio jambo ambalo tunatakiwa kulificha au kulipinguzia ukali wa maneno yake, nitoe rai kwa wasanii kwa ujumla kwamba ni kipindi ambacho wanapaswa kuangalia aina ya maisha wanayoishi, wajiepushe na matumizi ya dawa za kulevya na hata Wema naye ana jukumu sasa la kuwa mfano kwa jamii na kuhakikisha anakuwa Balozi mzuri kueleza madhara ya dawa za kulevya,” Wakili Msando

BREAKING: Wema amehukumiwa kwenda jela mwaka mmoja au faini Mil. 2

Soma na hizi

Tupia Comments