Habari za Mastaa

Kilichokataliwa leo na Mahakama kwenye kesi ya Wema Sepetu

on

Bado kesi ya Mwigizaji Wema Sepetu kuhusu bangi inaendelea kwenye Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es salaam ambapo leo ilikua ni siku nyingine tena kesi hiyo imeendelea.

Mpya ya leo ni kwamba Mahakama hiyo imekataa kupokea vielelezo vya ushahidi wa msokoto na vipisi viwili vya bangi vilivyotolewa na upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili Wema na wenzake.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo amesema Mahakama haiwezi kupokea vielelezo hivyo kwa sababu vina kasoro >>> “Nakubaliana na hoja kwamba msokoto wa bangi na vipisi vina kasoro kwa kuwa shahidi hakuvifafanua Mahakamani

Kesi hiyo imeahirishwa hadi September 12/2017.

VIDEO: Wema Sepetu asema Alikiba na Diamond ni wendawazimu, mtazame kwenye kila anachosema kwenye hii video hapa chini

RED CARPET: Wema na Idris wamerudiana??? mtu kashikwa mkono mwanzo mwishobonyeza play hapa chini kuona ilivyokua

IDRIS KAJIBU: Ni kweli amerudiana na Wema Sepetu? kupasha kiporo vipi? bonyeza play hapa chini kujionea

HAUTAKI KUPITWA??? Kuna hii APP MPYA YA MILLARD AYO kwa wewe wa ANDROID unaweza kubonyeza hapa moja kwa moja kwenda kui-download mtu wangu, HABARI ZOTE KIGANJANI MWAKO >>> APP MPYA BONYEZA HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments