Mix

Wizara ya Mambo ya Ndani imetangaza maamuzi haya kwa watumishi wake 14

on

Wizara mbalimbali za Serikali hii ya awamu ya tano zinazidi kuingia kwenye headline, ikiwa ni siku kadhaa zimepita baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga kuagiza idara ya uhamiaji ifanyiwe mabadiliko makubwa ili kuboresha huduma na kuimarisha uadilifu katika vitengo vya idara hiyo nyeti.

Leo March 18 2016 Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Idara ya Uhamiaji imefanya mabadiliko ya vituo vya kazi kwa maofisa 14 waandamizi katika Ofisi ya Makao Makuu, Mikoa, Wilaya na Vituo vya mipakani.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Kaimu Kamishna wa Utawala na Fedha Idara ya Uhamiaji, Abass Mussa Irovya ameleza kuwa hatua hiyo ya kubadilisha vituo ni endelevu na ni kwa maofisa zaidi ya mia mbili. Irovya amesema…>>> ‘Idara ya uhamiaji inaendelea na utaratibu wa kuwabadilisha vituo vya kazi Maofisa zaidi ya mia mbili kutoka sehemu mbalimbali nchini ikiwa ni Agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line yatiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard AyokwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE

ULIKOSA KITUKO KILICHOMCHEKESHA RAIS MAGUFULI IKULU JAPOKUWA ALIKUA KAWEKA SURA YA KAZI? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments