Habari za Mastaa

Alichokifanya Jackline Wolper kwenye Birthday ya KCEE wa Nigeria kimezua maneno

By

on

Ni haki yako kuzipokea habari zote zinazoendelea kutoka kwenye burudani mpaka hard news ndani na nje ya nchi ambapo leo April 18, 2017 stori nyingine iliyonifikia ni hii ya muigizaji staa wa Bongo movie Jackline Wolper kumpost muimbaji KCEE wa Nigeria.

Wolper ameposti picha hiyo kwenye account yake ya Instagram kwa dhumuni la kumtakia heri ya kuzaliwa msanii huyo kitu ambacho ni kawaida ambacho hufanywa na watu wengi, lakini kilichozua utata ni maneno aliyoandika kuambatana na picha hiyo.

>>>Happy birthday handsome
Always a good time with you
I gat mad love for you and you know it ??
God bless you @iam_kcee @iam_kcee akiwa anamaanisha “Heri ya siku ya kuzaliwa handsome. Siku zote nakuwa na wakati mzuri nawe. Nina upendo usioelezeka kwako na unafahamu.” – Jackline Wolper.

Kitu kingine kilichosababisha mashabiki kuongea ni baada ya Jackline Wolper kutoa picha yake kwenye DP yake ya Instagram (ile picha ya juu ambayo msanii anaweka kama utambulisho wake) na kuweka picha ya msanii huyo kutoka Nigeria.

 

Video: ‘Wimbo wa Niambie sijamuimbia Wolper, hii ni ya kila mtu’ -Harmonize >>>

Video: Taarifa za msiba wa Baba mzazi wa Belle 9>>>

 

Soma na hizi

Tupia Comments