Habari za Mastaa

Wolper kujifungua mtoto wa kiume Mchumba wake kathibitisha

on

Mwigizaji Jacqueline Wolper anatarajia kupata mtoto wa kiume, Rich Mitindo ambaye ni mchumba wake Wolper amethibitisha.

Rich amethibitisha leo hii May 7, 2021 kwa kupost kwenye ukurasa wake wa Instagram haya…>>>

Sijuii nieleze vip Furaha yangu, Ila ni wakati mzuri na  sitausahau kamwe kwenye maisha yangu.. jamaniii katika maisha yangu sijawahi kuwa na furaha na upendo kamili Kama ilivyokuwa wakati huu niseme nakupenda kuliko chochote katika ulimwengu huu, ilikuwa ndoto yangu kuwa na familia na sasa inatimia,

kwa hili nitashukuru milele Nakupenda Jacq wangu na nitampenda mwanangu sana sababu umembeba mwanangu ndani yako, nakuhahid nitakuwa baba bora mwaminifu kwako na mwenye upendo , na nitakuwepo na nyie milele 🙏 @wolperstylish “Rich Maitindo

Baada ya hapo AyoTV na millardayo.com zimezungumza kwa simu na mchumba wa Wolper, Rich ambaye amesema wanatarajia mtoto wa kiume ambaye watampa jina linaloanzia na herufi P.

PLAY hapa chini kupata taarifa kamili

Soma na hizi

Tupia Comments