Mix

Tanzania yanufaika na hizi bilioni kutoka Benki ya Dunia

on

Leo June 23 2016 Serikali imesaini makubaliano ya nyongeza ya fedha kwa ajili ya mfuko wa maendelea ya jamii TASAF, makubaliano ambayo yataifanya benki ya dunia iipatie Tanzania bilioni 440 kwa ajili ya kupeleka kwenye kaya maskini, kuwapatia ajira na kuhakikisha kaya hizo maskini zinapeleka watoto wao shule na kupata huduma za afya.

Katibu mkuu wa wizara ya fedha Dr. Servacius Likwelile amesaini mkataba huo kwa niaba ya serikali na kusema kuwa katika mwaka huu wa fedha mwaka 2015/2016 serikali na benki ya dunia imepitisha miradi 10 ambayo ina thamani ya trilioni 1.9 ambazo zitapelekwa katika miradi mbalimbali kama kuboresha kilimo, mradi wa kuimarisha umeme vijijini na elimu.

Aidha serikali ipo katika majadiliano na benki kuu ya dunia  katika kuboresha bandari ya Dar es salaam, miradi yote ikikamilika itagharimu kiasi cha trilioni 3.2.

ULIKOSA HII YA RAIS MAGUFULI KUELEZA SABABU YA KUSIMAMISHA AJIRA MPYA KWA MUDA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB INSTAGRAM YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments