Michezo

Maseneta Marekani walikataa Russia isiandae #WorldCup2018, FIFA imejibu hivi..

on

Russia-2018-600x353Hakuna uhusiano mzuri kati ya nchi ya Marekani na Russia, hiyo ilifanya baadhi ya Maseneta wa nchi hiyo kutaka FIFA izuie michuano ya Kombe la Dunia kufanyika Russia mwaka 2018.

March 2014 iliwahi kuripotiwa kwamba Seneta Mark Kirk na Dan Coates waliwahi kuandika barua kuiomba FIFA iifute Russia uanachama wa Shirikisho hilo la Soka.

Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano FIFA, Delia Fischer aliandika barua ya majibu ya ombi hilo kwamba FIFA haiko tayari kukubaliana nao; “The boycott of sports or policies of isolation or confrontation are not the most effective ways of solving problems“.

Maseneta hao pamoja na John McCain ambaye aliwahi kugombea Urais wa Marekani 2012, waliandika barua FIFA kuliomba Shirikisho hilo kuizuia Russia kuandaa michuano ya World Cup 2018.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments