Unamkumbuka Hawa aliyeshirikishwa kwenye wimbo ‘Nitarejea’ wa Daimond Platnumz? Amefunguka na kuelezea namna hali yake ilivyobadilika na jinsi alivyoanza kutumia pombe kali huku akikiri kuwahi kuwa mapenzini Diamond.
Kwenye The Weekend Chart Show ya Clouds TV Hawa amesema mtoto aliyenaye sio wa Diamond bali wa mwanaume mwingine aliyemjua kupitia Maunda Zorro ingawa mama yake mdogo akidai mama mzazi wa Diamond alishawahi kwenda nyumbani kumuona akihisi ni mtoto wa Diamond.
>>>”Diamond nilikuwa natoka naye tumeshaishi kabisa. Sasa hivi sitamani, mapenzi yapo na kuna kuisha japo natamani lakini siyo riziki yangu. Nyimbo zake naziimba lakini siyo kwamba namchukia. Najaribu kumtafuta na WCB napajua nilishaenda nikaambiwa Diamond amesafiri. Nilienda anichangie kadi ya harusi.
“Sijui naumwa kitu gani ila nahisi kutokana na pombe. Sasa hivi sijanywa na kunywa dawa. Pombe ninazokunjwa mimi ni za kienyeji ilimradi kuyumba tu. Kitu kilichonisukuma ni makundi ambayo nakaa nayo na mawazo pia.
“Kunywa gongo sijui nilianzaje lakini wakati nilipokuwa nakaa kwa Maunda katika harakati za kujifunza muziki kwa kuwa nilikuwa napenda muziki. Kule wanakunywa pombe ndio nikaanza na aliyeninunulia pombe ni baba yake huyu mtoto. Alivyoondoka akaniacha nikawa nimeshazoea pombe.
“Mimi nikabaki na arosto ya kukosa pombe halafu sina hela ikabidi nianze kunywa pombe za bei rahisi lakini pia mapenzi nayo yalichangia sana ya baba yake huyo mtoto sio Diamond.” – Hawa.
Naye mama mzazi wa Hawa alionesha kusikitishwa na hali ya binti yake akisema alikuwa anamkataza sana lakini hakumsikiliza.
.>>>“Anakunywa gongo huyo. Nilishamkataza sana mwanangu huyo. Kila siku nalia, ninamuomba Mungu usiku silali kuhusu huyu mtoto. Ananitia uchungu sana hata ukituangalia sasa hivi mimi na yeye nani mama? Mimi ni mama lakini mzazi akikuambia kitu usifanye wewe usifanye mwanangu hanielewei.” – Mama mzazi wa Hawa.
Bonyeza Play hapa chini kusikiliza Full Story …
“Naomba Serikali ilegeze kidogo ili mashabiki wangu wafurahi” – Snura