Leo inawezekana ikawa ni siku ya kihistoria kwa staa wa Tanzania anayeichezea timu ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta, nahodha huyo wa Taifa Stars licha ya kufunga goli mbili katika ushindi wa goli 5-2 wa KRC Genk dhidi ya KAA Gent katika mchezo wa 16 bora wa Europa League, amechaguliwa katika kikosi bora cha wiki.
Samatta ametajwa katika kikosi bora cha wiki cha UEFA Europa League kwa mara ya kwanza katika historia lakini ametajwa pia na staa mwenzake wa KRC Genk ambaye pia ni nahodha wao msaidizi wa Genk Pozuelo na mchezaji mwenzao Malinovskiy.
Jina la Samatta linakuwa ni miongoni mwa majina 11 kutoka katika baadhi ya timu 16 ambazo zina zaidi ya jumla ya wachezaji 176, waliyoonekana kufanya vizuri katika usiku wa round ya kwanza wa Europa League hatua ya 16 bora, kwa upande wa Man United staa wao Henrikh Mkhitaryan ndio katajwa katika list hiyo.
VIDEO: ALL GOALS: Simba vs Yanga February 25 2017, Full Time 2-1