Habari za Mastaa

Kitu Wema Sepetu ameandika kuhusu yeye na familia yake

By

on

February 13, 2017 kupitia Instagram ya staa mrembo Wema Sepetu leo ameandika kitu kuhusu yeye na familia yake pamoja na kuwashukuru watu wote walioshirikiana naye wakati akiwa kwenye kipindi kigumu, pia amewakumbusha mashabiki zake kudownload App yake ambayo inapatikana hapa.

Wema Sepetu ameandika hivi leo.

“Mimi na familia yangu tunapenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani zetu za dhati kwa wote mlioshirikiana nasi kwa hali na mali katika kipindi hiki kigumu tulichopitia. Najua wengi mlikua mnaniombea, nashukuru kwa sala na dua zenu kwani zimenisaidia kwa kunipa nguvu wakati nikiwa kwenye wakati mgumu sana kwenye maisha yangu”.

“Napenda kuwashukuru mashabiki wangu wote duniani kwa kuniamini na kusimama na mimi kwa kipindi chote hiki, pia napenda kuwashukuru wasanii wenzangu wote”.

“Asante sana kwa mwanasheria wangu Alberto Msando kwa kunisimamia na kuwa na mimi bega kwa bega wakati huu mgumu. Nakuombea kwa Mungu akupe moyo huohuo wa kuwatetea wanyonge. Asante sana. Familia ya marehemu Mzee Issac Sepetu tunasema asanteni sana”.

#WemaApp hakikisha umedownload kutoka Playstore afu tuongee kule zaidi..

VIDEO: Sababu za Wema Sepetu kuzifuta picha zote Instagram amezieleza hapa. Bonyeza play kutazama.

Soma na hizi

Tupia Comments