Duniani

UTAFITI: Manyanyaso kwa mtoto husababisha kubalehe mapema

on

Wataalamu wa Saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Penn State, Marekani wamegundua katika utafiti wao kuwa zaidi ya 90% ya watoto waliopitia maisha ya kunyanyaswa, kupigwa au kudhalilishwa kingono wanabalehe haraka ukilinganisha na watoto wanaolelewa kwa upendo.

Professor Jennie Noll aliliambia Jarida la Adolescent Health: >>> Watoto hasa wa kike wanaolelewa kwa kunyanyawa hasa kupigwa au kubakwa hubalehe kabla ya muda ukilinganisha na watoto wanaolelewa kwa upendo pia watoto wa aina hii huota matiti mapema ukilinganisha na watoto wa kawaida.

Akielezea uhusiano ulipo baina ya mtoto kunyanyaswa na kubalehe kabla ya wakati Dr. Noll alisema watoto wanaokuwa katika mazingira kama hayo huzalisha homoni nyingi zinazotokana na msongo mkubwa wa mawazo hivyo kuharakisha muda wa balehe.

Wanasaikolojia hao pia walisema mtoto anayenyanyaswa yuko hatarini zaidi kupata saratani ya ovari na matiti ukilinganisha na watoto ambao hulelewa kwenye mazingira ya upendo na amani.

ULIKOSA? Eti mwanamke kunyonywa matiti na mwanaume inapunguza maambukizi ya kansa?  Bonyeza play kuitazama.

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo

 

Soma na hizi

Tupia Comments