Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia General Mstaafu Emmanuel Maganga ameongoza zoezi la ufunguzi wa sanamu ya samaki aina ya Mgebuka iliyozinduliwa katika Manispaa ya Kigoma ujiji ikiwa ni sehemu ya utambulisho wa Rasilimali za mkoa huo.
Katika zoezi hilo mamia ya wakazi wa Mkoa wa Kigoma wamejitokeza kushuhudia ufunguzi wa sanamu hiyo ambayo imejengwa eneo la Mapandanjia ya barabara ya soko la Mwanga kwenda Kigoma Mjini na Ujiji ambapo kabla ya uzinduzi Meneja wa TANROAD Mkoa wa Kigoma Engineer Naris Choma amesema mpaka kukamilika imetumika zaidi ya Milioni 100.
KIJANA ALIEFELI MASOMO, ANAYO CARWASH INAYOTEMBEA, KAJENGA NYUMBA