Top Stories

Mwongozo kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano.

on

Wajibu mmojawapo wa watumiaji wa huduma ni kuunga mkono usimamizi; ambao kwa sekta ya mawasiliano hapa Tanzania unafanywa na TCRA. Mamlaka imetoa Mwongozo huu kama sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka katika kutoa elimu kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kwa wakati huu.

Sekta ya mawasiliano inakua na kubadilika; ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa huduma na bidhaa
na kwa mantiki hiyo pia watoa huduma na watumiaji na kutokuwepo kwa baadhi ya huduma na bidhaa.

Kasi ya kukua na kubadilika kwa tekinolojia ya mawasiliano ni kubwa; na msimamizi, mtoa huduma na mtumiaji hawana budi kuendana nayo. Huduma na bidhaa zilizotolewa maelekezo ya matumizi katika Mwongozo huu zinabadilika.

Hivi sasa, tekinolojia inaelekea kwenye matumizi makubwa ya mtandao wa intaneti kwa shughuli nyingi za kibinafsi na kitaasisi. Kupitia intaneti, watu na taasisi wanaweza kuwasiliana na vifaa vya mawasiliano nakuvipa vyombo hivyo maelekezo ya kitu cha kufanya. Miaka michache ijayo kutakuwa na ongezeko la mitandao ya vyombo vinayowasiliana baina yao moja kwa moja kupitia intaneti.

Hali hii italeta fursa na changamoto nyingi kwa watumiaji na watoa huduma. Kutakuwa na fursa za kiuchumi na kuongezeka kwa ufanisi. Baadhi ya changamoto zitatokana na fursa zenyewe, matumizi ya huduma na bidhaa hizi na upeo wa uelewa wa jamii. Katika hali hii, kutakuwa na umuhimu wa kutoa elimu ya ziada kwa wadau.

Masuala yaliyozungumziwa kwenye Mwongozo huu yameelezewa kwa kirefu kwenye maandishi mbalimbali ambayo TCRA inayatumia kama sehemu ya kutoa elimu kwa umma na kwa watumiaji. Aidha machapisho yanayofafanua kwa undani vipengele vyote kwenye Mwongozo huu yanapatikana makao makuu ya Mamlaka Dar es Salaam, Ofisi ya Zanzibar, ofisi za Kanda na pia kwenye tovuti ya TCRA ambayo ni www.tcra.go.tz

Mwongozo huu utapitiwa mara kwa mara ili uweze kukidhi matarajio ya watumiaji na matakwa ya
usimamizi kwa wakati husik

Soma na hizi

Tupia Comments