Ad
Ad

Mix

Headlines za Kylie Jenner kurudiana na mpenzi wake wa zamani Tyga

on

NI Mrembo mwenye umri wa miaka 20 kutoka kwenye familia ya Kardashian Kylie Jenner ambae hivi karibu aliziandika headlines mitandaoni za kuachana na Baba wa mtoto wake, Travis Scott.

Sasa usiku wa kuamkia  October 2, 2019 Mrembo huyo Kylie Jenner alionekana akiwa anaingia pamoja na rafiki zake wawili kwenye hotel ya Sunset Marquis huko Los Angeles Marekani ambayo ndani yake kuna studio ambazo alikuwa anazitumia mpenzi wake wa zamani Tyga.

Inadaiwa Kylie na marafiki zake wa kike waliotambulika kwa majina ya Kelsey Calemine na Stassi walionekana wakitoka katika hoteli hiyo na baadae muda mfupi  Rapper Tyga na Kylie walionekana wakipita mlangoni wa nyuma ili kuwakwepa waandishi wa habari waliofika nje ya hoteli hiyo.Hivyo imepelekea mijadala mbalimbali mitandao kwamba wawili hao wamerudiana.

Aidha mitandaoni imeripoti kwamba Travis Scott ndio chanzo cha kufanya Kylie Jenner avunje uhusiano wao kwani inadaiwa Travis Scott alikuwa kwenye uhusiano wa kimya kimya takribani miaka 9 na mrembo mwingine bila Kylie Jenner kutokujua chochote.

Kylie na Travis Scott walifanikiwa kupata mtoto aitwae Stormi Webstar.

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments