AyoTV

VIDEO: Exclusive ya Waziri Nape kuhusu wabunge wa upinzani wanaosusia bunge

on

Katika exclusive interview na AYO TV nakukutanisha na Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye akizungumzia kitendo cha baadhi ya wabunge wa upinzani bungeni kususia vikao vya bunge kwa madai ya kutokuwa na imani na Naibu spika Dk. Tulia Ackson.

Waziri Nape amesema…>>>’Wingereza wanasema mtu mwenye akili ndogo anajadili watu, wenzetu wana mgogoro na naibu spika lakini zipo njia za kibunge za kutatua huu mgogoro lakini wao hawataki kuzifuata, hii ni ishara kuwa wanaongozwa na akili ndogo

Lakini la pili kubwa linalosikitisha ni kuwa anayewaongoza kutoka na kuingia Freeman Mbowe haji, havai makaratasi kama wenzake na huwenda yupotu nyumbani amelala nyumbani kwake. Ushauri wangu wajaribu kuwa na akili kubwa kidogo ya kushughulika na mfumo‘ –Waziri Nape Nnauye

Baya kuliko yote ni kwamba wanawanyima fursa watu waliowachagua, utaona wameuliza maswali ambayo ilitakiwa yajibiwe na wao wakiwepo na hii ni salamu kwamba katika uchaguzi ujao tuweke watu ambao watajua wametumwa na wananchi‘ –Waziri Nape Nnauye

ULIIKOSA HII YA WAZIRI MWIJAGE AKIWAJIBU WANAOSEMA KAPEWA BAJETI KIDOGO

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa  INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments