Top Stories

RC Makonda kazindua ujenzi wa Ofisi 402 za Walimu, DSM

on

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo September 19, 2017 amezindua rasmi zoezi la ufyatuaji wa matofali na kushiriki kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za kisasa 402 za Walimu akiwasihi wadau na Wananchi kuunga mkono jitiada hizo.

RC Makonda amesema lengo la ujenzi wa Ofisi hizo ni kuboresha mazingira ya kufanya kazi kwa walimu ili watoa elimu bora kwa Wanafunzi na kuongeza ufaulu akisema wengi walipanga kufanya ujenzi wa Ofisi za Walimu lakini mipango iliishia kwenye makabrasha maofisini lakini kupitia juhudi zake na Kamati aliyoiunda wameweza kuleta matokeo chanya.

RC Makonda ametoa wito kwa wananchi na wadau kuchangia ujenzi huo kwa vifaa na nguvu kazi ili kuwawezesha walimu kufanya kazi katika mazingira bora.

Aidha, ameipongeza Kamati ya ujenzi wa Ofisi hizo, JKT, Jeshi la Magereza, Jeshi la Polisi, NHC, TBA, Channel Ten na Umoja wa Wamiliki wa Malori na wengine kwa namna wanavyojitoa kusaidia katika zoezi hilo.

FULL VIDEO: Makonda, Ruge na Wahariri wazungumza kwa pamoja na Waandishi

BREAKING: RC Makonda katangaza kupunguza bei ya viwanja DSM

Soma na hizi

Tupia Comments