Habari za Mastaa

NEW YORK! 50 Cent kadai alipewa ofa ya fedha ampigie Kampeni Trump

on

Rapper Curtis ’50 Cent’ Jackson amedai wakati wa kampeni za Mgombea Urais wa Marekani Donald Trump alipewa ofa ya Dola 500,000 ili kumsaidia wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Akizungumza katika interview na Radio Hot 97 ya New York, Jackson alisema, wakati wa kampeni za Trump, alipewa ofa ya Dola 500,000 kwa kile alichodai kuongeza nguvu ili kuzipata kura za Wamarekani weusi.

>>>”Ilikuwa kama hapana, sio fedha nzuri. Sitofanya hivyo…hazina thamani.”

Cent, ambaye alikuwa ana-promote show yake ya TV inayoitwa Power, pia aliita uchaguzi wa Trump kama ‘ajali.’

>>>”Kama unakuwa Rais kwa bahati mbaya, utafanya baadhi ya mambo kama afanyayo Donald Trump. Nadhani alikuwa anafanya kampeni ya kutengeneza wasifu wake.”

Mwaka 2015, 50 Cent aliwahi kunukuliwa na The Daily Beast kuwa anamuunga mkono aliyekuwa Mgombea Urais Hillary Clinton, akisema nafasi hiyo ilimfaa kwa sababu ya uwepo wake Ikulu wakati wa Urais wa mumewe Bill Clinton.

PARTY YA DIAMOND: Pre-Birthday ilivyopendeza DSM na alivyoimba ‘Hallelujah’

Soma na hizi

Tupia Comments