RAIA wa Uholanzi Monique Amanzi mwenye umri wa miaka 28 anayekabiliwa na tuhuma za kuishi nchini bila kibali leo September 22, 2017 ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa alichaniwa Passport yake na Ofisa wa Polisi kitengo cha Usalama Barabarani (Trafiki).
Amanzi ambaye pia anahusishwa na biashara ya kujiuza, alisomewa kosa lake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa na Wakili wa Uhamiaji Novatus Mlay ambapo Wakili huyo alidai kuwa September 11, 2017 Idara ya Uhamiaji Makao Makuu, Kurasini Temeke ilimbaini kuwa anaisha nchini kinyume na sheria.
Baada ya kusomewa Amanzi alikana kosa, ambapo alidai kuwa rafiki yake wa kiume ambaye ni Polisi Kitengo cha Usalama wa Barabarani anayefanya kazi maeneo ya Victoria Makumbusho alichana hati yake ya kusafiria akidai baada ya kuchanwa kwa hati hiyo aliripoti Polisi Kinondoni miaka miwili iliyopita lakini alipoteza RB na kwamba ana watoto watatu ambapo mmoja amefariki.
Miongoni mwa watoto hao wawili ni wa mume wake Ibrahimu Abas ambaye alikuja nae hapa nchi lakini walitengana na kumpata Trafiki ambaye alizaa naye mtoto mmoja bahati mbaya akafariki.
Alidai kuwa aliwahi kwenda Uhamiaji lakini hakupata mafanikio.
Dhamana ya mshtakiwa iko wazi ambapo anatakiwa kuwa na wadhamini wawili raia wa Tanzania ambao kila mmoja atasaini bondi ya Tsh Milion Moja ambapo hata hivyo, upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na Hakimu Nongwa aliahirisha kesi hadi Septemba 27, 2017 kwa ajili ya kutajwa.
BREAKING: Mbowe asema alipo Dereva wa Lissu na kwanini hakuripoti Polisi