Top Stories

UPDATES! Zitto katolewa Polisi, amepelekwa Ofisi za Bunge kuhojiwa

on

Baada ya taarifa za kukamatwa kwake jana akiwa Airport DSM kisha mapema leo kutolewa taarifa nyingine za kufikishwa Dodoma chini ulinzi wa Polisi na kuwekwa Central Police Dodoma, zipo taarifa nyingine za muda huu kuwa Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amepelekwa katika Ofisi za Bunge.

Taarifa ya ACT Wazalendo mchana huu zinaeleza kuwa Zitto Kabwe ametolewa Ofisi ya Polisi Mkoa wa Dodoma alikoshikiliwa tangu saa tatu asubuhi na sasa amepelekwa katika Ofisi za Bunge kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Zitto atahojiwa mbele ya Kamati hiyo ambayo inaongozwa na Mbunge wa Newala George Mkuchika.
Endelea kukaa karibu na millardayo.com na APP mpya ya ‘millardayo‘ kwa wenye simu za ANDROID ili kupata kila kitachonifikia.

ULIPITWA? Zitto Kabwe kafikishwa Dodoma, amewekwa Central Police!!

Soma na hizi

Tupia Comments