Xabi Alonso anahisi kwamba Cristiano Ronaldo hakuwa sahihi na alichangia katika kujisababishia kadi nyekundu katika mchezo wa matokeo ya 1-1 baina ya Real Madrid vs Athletic Bilbao mechi iliyochezwa jana usiku.
Mwanasoka huyo bora wa dunia alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kukwaruzana na Carlos Gurpegui na Ander Iturraspe katika dakika ya 76 ya mchezo, lakini Alonso anasema mwamuzi Miguel Ayza alifanya maamuzi ya kumtoa Ronaldo kwa presha kutoka kwa mashabiki.
“Cristiano hakupaswa kufanya alichofanya, lakini halikuwa kosa la kutolewa nje kwa kadi nyekundu,” Xabi Alonso aliwaambia waandishi wa habari.
“Kosa lile lilikuzwa, refa Gurpegui alishinikizwa na presha kutoka kwa mashabiki, hili sio jambo jipya hapa.”
Sare ya jana iliisogeza Madrid kuwa sawa kwa pointi na Barcelona huku wakiwa nyuma kwa pointi 3 kutoka kwa wanaongoza ligi Atletico Madrid.