Philipp Lahm alimuunga mkono kocha wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso siku ya Jumanne kufanya uamuzi sahihi kuhusu mustakabali wake, akimtaja mchezaji mwenzake wa zamani wa Bayern Munich kuwa “mwanamkakati”.
“Xabi Alonso amekuwa mtaalamu wa mikakati. Unaweza kutabiri kuwa atakuja kuwa kocha mkuu,” Lahm aliiambia AFP katika mahojiano.
Lahm alicheza na Alonso kwa miaka mitatu huko Bayern, na wote wawili walistaafu msimu wa joto wa 2017.
Lahm sasa ni mkurugenzi wa mashindano kwa wenyeji wa Euro 2024 Ujerumani, wakati Alonso ameibuka kuwa mkufunzi mkali zaidi katika soka.
Leverkusen ya Alonso iko mbioni kunyakua taji la kwanza kabisa la Bundesliga, wakiwa wamekaa pointi 10 mbele ya Bayern kwenye ligi hiyo zikiwa zimesalia mechi nane.
Bila kushindwa katika michuano yote, Leverkusen wamefanikiwa kutinga nusu fainali ya Kombe la Ujerumani na nane bora ya Ligi ya Europa.