Chama cha Wananchi CUF upande wa wanaomuunga mkono Mwenyekiti Prof Ibrahim Lipumba umetangaza kusimamisha wagombea 43 katika Kata zote wakati wa Uchaguzi mdogo wa Madiwani unaotarajia kufanyika November 26, 2017.
Aidha, Chama hicho, kimesema hakitashirikiana na UKAWA katika chaguzi hizo bali kitasimamisha wagombea wake kama chama cha siasa.
Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Mkurugenzi Mipango na Uchaguzi (NMCO), Mneke Jafar amesema, CUF kimepokea barua ya Uchaguzi mdogo wa Madiwani kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi ‘NEC’ ambapo kimefanya upembuzi yakinifu kuhusu uchaguzi huo na kuamua kusimamisha wagombea Kata zote 43.
>>>”CUF imejipanga vizuri na kitasimamisha wagombea wazuri wenye uzalendo wa kweli wa kuwatumikia Watanzania katika Kata hizo. Pia chama kinaendelea kupokea wanachama wapya kutoka vyama mbalimbali.”
Mbali na hilo pia Jafar amesema wanatoa onyo na karipio kali kwa wale wenye tabia ya kujipachika vyeo feki kwa anuani ya CUF akisema:>>>”Wananchama wasikubali tena kuona nembo za Chama zikichezewa na mtu ama Chama chochote kile.”
Amewataka Wanachama kupuuza propaganda kwamba kuna Wabunge wameshinda kesi na yamebaki machache kuapishwa.
Aidha, Jafar amesema chama hicho hakitashirikiana na Umoja wa Katiba ya Wananchi ‘UKAWA’ kwa sababu ushirikiano uliokuwepo wakati wa uchaguzi Mkuu 2015:>>>”Lengo la Chama cha siasa ni kushika Dola, hivyo mpuuzie taarifa kwamba tutashirikiana na UKWA. Sisi tutasimamisha wagombea wetu.”
BREAKING: Tamko la CUF ya Maalim Seif kuhusu wabunge 7 walioapishwa