Mbunge wa Mikumi Joseph Haule ‘Professor Jay’ ni miongoni mwa mahanga wa zoezi la bomoabomoa linaloendelea ambalo linafanywa na TANROADS kuondoa nyumba zilizopo ndani ya hifadhi ya barabara ili kupisha upanuzi wa barabara ya Morogoro.
Baada ya tukio hilo, kupitia Instagram yake, Professor Jay alieleza namna alivyosikitishwa na zoezi hilo lililotokea wakati yupo kwenye majukumu yake ya kibunge kwenye Jimbo la Mikumi.
>>>”Mimi ni mmoja wa wahanga wa hili zoezi la kubomolewa nyumba zetu huku Mbezi Kimara Tarehe 29/9/ 2017. Jana nikiwa katika majukumu jimboni Mikumi Majira ya saa kumi mbili hivi jioni, nilitaarifiwa kwamba, watu wa Tanroads wakiwa wameambatana na grader mbili na magari mawili ya polisi (defenders) yenye askari waliokuwa na silaha mbalimbali za moto walikuwa wanabomoa nyumba yangu.
“(sijawahi kuumia kiasi hiki ?) Nimesikitishwa sana jinsi Tanroads wanavyoweza kujichukulia maamuzi bila ya kujali mhimili muhimu wa Mahakama wametoa maagizo gani. ? Na taratibu zilizotumiwa kubomoa nyumba yangu bila ya mimi na Tanesco kupewa taarifa saa kumi na mbili jioni (haukuwa muda wa kazi) na kubomoa huku Umeme ukiwa unawaka ni kitendo ambacho kwanza kina hatarisha maisha ya wabomoaji wenyewe, maisha ya familia yangu pamoja na majirani zangu , LIMENISIKITISHA zaidi.
“Nasema hivi kwasababu Tanesco wamenipigia simu baada ya masaa 24 au zaidi baada ya zoezi la kubomoa nyumba kufanyika kunitaarifu kuja kukata Umeme kabla ya ubomoaji huo, pindi nilipo waambia kwamba mbona nyumba IMESHABOMOLEWA kabisa na sijaweza kuokoa kitu chochote na hata hiyo meter yenu mnayoiulizia mkaitafute kwenye kile kifusi cha nyumba yangu kilichokusanywa kwa pamoja na watu wa Tanroads. Tanesco walishangazwa sana kuvunjwa nyumba yangu kwa taratibu hizo.
“Lakini naamini kila kitu kinatokea kwa sababu maalum. Nimejifunza kumtegemea Na kumshukuru Mungu kwa kila jambo. Na hili ni moja ya mitihani ya hapa duniani. Nimepokea na kumsikiliza Mungu ana mipango gani juu yetu katika familia yangu mbeleni. Tumelipokea na Naamini tutashinda ??.”
Kimara wanavyolala nje baada ya bomoabomoa
ULIPITWA? BOMOA BOMOA DAR: Wakazi Kimara waeleza wanavyoishi kwa shida…tazama kwenye hii video hapa chini!!