Michezo

FC Barcelona wanaibomoa Atletico Madrid

on

Mshambuliaji tegemeo wa club ya Atletico Madrid ya Hispania Antoine Griezmann ametangaza kuwa anaondoka katika club hiyo usiku huu, Griezmann ametangaza rasmi kuwa anaondoka Atletico Madrid lakini hajaweka wazi club gani anakwenda.

Muda mchache kabla ya taarifa zake kutoka kuwa anaondoka ndani ya club hiyo, mwandishi wa habari wa Hispania Fabrizio Romano alitangazwa kuwa staa huyo anaondoka na kwenda katika club ya FC Barcelona ya Hispania ambayo tayari imetenga mezani dau la euro milioni 125.

Kama kweli FC Barcelona watakamilisha usajili huo basi watakuwa wanaibomoa safu ya ushambuliaji ya Atletico Madrid kwa kiwango kikubwa, Griezmann amekuwa nguzo muhimu ya ushambuliaji ya Atletico Madrid toka 2014 alipojiunga nayo akitokea Real Sociedad ya nchini humo, Griezmann mwenye umri wa miaka 28 kwa sasa inaelezwa atapewa mkataba wa miaka mitano na FC Barcelona.

Mzee Muchacho na Fahad wambananisha Haji Manara avae jezi ya Yanga SC

Soma na hizi

Tupia Comments