Mix

Ofisi ya Bunge yamjibu Mbowe kuhusu fedha za matibabu ya Lissu

on

September 22, 2017 Taarifa kutoka Ofisi ya Bunge imeeleza kuwa kiasi cha fedha Tsh Milioni 43 zilizochangwa na Wabunge kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, tayari zimetumwa katika akaunti ya Hospitali ya Nairobi anakotibiwa.

Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa fedha zimetumwa tangu September 20 na kusema ilichelewa kwa sababu ya taratibu za mawasilino ya kupata namba ya akaunti.

Taarifa hiyo ya Bunge imekuja muda mfupi baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA kukutana na Waandishi wa Habari leo ambapo pamoja na mambo mengine, alisema kuwa mpaka sasa pesa zilizochangwa na Wabungwe kwa ajili kuchangia matibabu ya Lissu hawajazipata.

 

Freeman Mbowe karudi Dar, aongelea yote ya Tundu Lissu kwa mara ya kwanza

Soma na hizi

Tupia Comments