Jumatatu, October 2, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesisitiza kuwa Afisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Temeke, (RCO) lazima afike Mahakamani hapo ili aeleze wamefikia wapi kuhusu upelelezi wa kesi ya mauaji inayomkabili mke wa marehemu Bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na mfanyabiashara Revocatus Muyela.
Hatua hiyo inatokana na Wakili wa utetezi Peter Kibatala kumueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa RCO aitwe ili aeleze upelelezi ulipofikia.
Awali, Wakili wa Serikali Estazia Wilson alidai shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi unaendelea ambapo baada ya kueleza hayo Hakimu Simba alisisitiza RCO aitwe Mahakamani na kuahirisha kesi hiyo hadi October 16, 2017 kwa ajili ya kutajwa.
Washitakiwa hao Februari 23, 2016, waliachiwa huru na Mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa kisha kukakamatwa tena na baadaye kusomewa mashtaka hayo ya mauaji upya.
Katika kesi hiyo namba 5/2017 wanadaiwa kumuua kwa makusudi Dada wa marehemu Bilionea Erasto Msuya, Aneth Msuya tukio linalodaiwa kufanywa May 25, 2016 maeneo ya Kibada, Kigamboni Dar es Salaam.
JOSHUA NASSARI: “Hii Tamthilia bado inaendelea”