Wilaya ya Karagwe ni miongoni mwa maeneo yanayokabiliwa na changamoto ya maji ambapo wananchi hulazimika kutembea umbali mrefu kutafuta huku wakishindwa kutekeleza majuku mengine ya kimaendeleo kwa muda muafaka.
Good news ni kwamba, ili kuwasaidia wananchi kutotembea umbali mrefu kutafuta maji na kushindwa kufanya shughuli nyingne za kimaendeleo kwa wakati, changamoto hiyo imeanza kufanyiwa kazi baada ya Shirika la Tumain Fund na Rotary Club ya Marekani kujenga visima vya maji zaidi ya 10 ambavyo vina thamani ya Tsh Million 360 ambapo vitahudumia Wakazi wa Kata za Kituntu na Kanoni na maeneo jirani.
Baada ya uzinduzi wa mradi huo Mkuu wa Wilaya Karagwe, Godfrey Mheruka amewataka wananchi wa maeneo hayo kuhakikisha wanaulinda mradi huo huku akiwataka walionzisha shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji kuhakikisha wanaondoa mazao yao ili visikauke.
Godbless Lema awaonya Polisi “Nimeapishwa juzi na Rais Magufuli”