Top Stories

Mwanamke aliyehukumiwa miaka 15 jela kwa kuwa mapenzini na Mwanafunzi

on

MWANAMKE mmoja mwenye umri wa miaka 26 jana Jumanne alihukumiwa na Mahakama ya Kitale, Kenya, kifungo cha miaka 15 jela baada ya kujihusisha kimapenzi na mvulana wa miaka 17.

Jane Gichuhi, anadaiwa kwa makusudi alijihusisha kimapenzi na mvulana wa miaka 17 ambaye ni mwanafunzi wa Kidato cha Tatu kati ya April 26, 2015 na May 11, 2015 katika eneo la Machinjoni, Kauti ya Trans Nzoia.

Kwa mujibu wa mlalamikaji, ambaye ni mwanafunzi wa Friends Bwake Secondary School katika Mji wa Kitale, alidai kulazimishwa kufanya mapenzi baada ya kumuomba urafiki.

Katika kujitetea kwake, mtuhumiwa alidai ni mgonjwa pia ana mtoto mdogo akiiambia Mahakama pia kuwa anategemewa na familia na ana madeni ambayo anatakiwa kulipa.

Hata hivyo, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Grace Sitati alimhukumu mtuhumiwa huyo kifungo cha miaka 15 jela na kusema mtuhumiwa anazo siku 14 za kukata rufaa.

UBUNIFU: Mtanzania aliyetengeneza spika zenye jina lake

Soma na hizi

Tupia Comments