Top Stories

GOOD NEWS! Bruce Wills kathibitisha kuendelea na DIE HARD 6

on

MWIGIZAJI staa wa filamu za Hollywood Bruce Willis ametia saini kukubali kuendelea na kuigiza katika mfululizo wa filamu ya DIE HARD akiwa kama Askari akitumia jina la John McClane ambayo sasa inaandaliwa Namba sita, Die Hard: Year One.

Muogozaji Len Wiseman, ambaye alisaini kuiongoza sehemu iliyopita, amesema filamu mpya ijayo itamuonesha McClane katika muonekano tofauti wa zamani na sasa, kwa mujibu wa Deadline.

Baadhi ya sehemu ya movie itamuonesha McClane ‘Bruce Wills’ akiwa kijana Askari kijana akifanya kazi katika Jiji la New York City miaka ya 1970. Wiseman amesema tayari wameanza kuandaa mazingira ya kumtengeneza McClane kijana na sehemu nyingine ya movie itamuonesha Willis akicheza nafasi yake kama McClane.

Toleo lililopita la movie hiyo, “A Good Day to Die Hard,” iliingia sokoni mwaka 2013, haikufanya vizuri Marekani lakini ilipata soko sehemu nyingine duniani.

Pamoja na kukubali kuigiza toleo la sita la Filamu hiyo, mwaka 2010, Willis alinukuliwa na Showbiz Spy kuwa atastaafu kuigiza mfululizo huo baada ya toleo la sita.

>>>”Miaka michache ijayo watamtafuta mbadala wangu au watamuita mhusika jina lingine. Lakini mimi, nitafanya Die Hard 5, kisha movie ya mwisho ya Die Hard — Die Hard 6 — kabla ya kustaafu. Sasa hivi naweza kukimbia na kupigana kwenye screen. Lakini utafika wakati sitaweza kufanya hivyo. Ndipo nitakaa kando na filamu za Die Hard.”

Bruce alicheza filamu ya kwanza ya Die Hard mwaka 1988 akitumia jina la John McClane na tangu hapo amekuwa akiendelea na matoleo mengine; Die harder 1990, Die Hard With A Vengeance 1995, Live Free Or Die Hard 2007, na A Good Day To Die Hard 2013.

Kitu RC Mwanza ameagiza baada ya kukagua Shule ya Bukongo, Ukerewe

Soma na hizi

Tupia Comments