Good news kwa mashabiki na wapenzi wa Rush Hour! Staa wa sanaa za mapigano wa China, Jackie Chan amethibitisha kwamba Rush Hour 4 ipo katika hatua za awali za utayarishaji wake, lakini kuna kigezo kimoja: Chris Tucker anahitaji kukubali kusaini kwenye project.
Akizungumza katika kipindi cha Power 106’s The Cruz Show, Jackie Chan mwenye umri wa miaka 63 sasa aliulizwa kama subira ya muda mrefu ya mashabiki itawafikisha kwenye muendelezo wa cinema hiyo alisema. “Kwa kipindi cha miaka saba tumekuwa tukiikataa script, kuikataa script… jana tumekubali. Huenda mwisho wa mwezi huu watakuwa na pendekezo la pili. Mwaka ujao wataanza, natumai – kama Chris Tucker atakubali.”
Kama ni mfuatiliaji mzuri wa Rush Hour, utakumbuka filamu ya kwanza ya Rush Hour ambayo ilitoka 1998, Jackie Chan alicheza kama inspector Lee kutoka Hong Kong, ambaye aliungana na Tucker kumuokoa binti wa balozi. Baada ya filamu hiyo, ikafuatia Rush Hour II ambayo ilitoka August 3, 2001 kabla ya kuachia Rush Hour III iliyoingia sokoni August 10, 2007 ikiwa ni miaka 10 sasa.
Watu wengi walioifuatilia walikuwa wanahoji iwapo kutakuwa na muendelezo wa Rush Hour IV kutoka kwa mastaa hao na alipoulizwa Jackie Chan alisema tatizo haliko katika fedha za kuandaa filamu hiyo bali muda: “Ni kuwa na muda wa kufanya [Rush Hour 4]. Vinginevyo, tutakuwa wazee. Nilimwambia Chris Tucker, ‘Kabla hatujazeeka, tafadhali fanya Rush Hour 4’.”
DIWANI MWINGINE KAWAJIBU LEMA NA NASSARI, KATOA SIKU SABA