Top Stories

MLIPUKO KAGERA: Wanafunzi 45 wajeruhiwa

on

Mapema leo November 8, 2017 kulisambaa taarifa kutokea Kanda ya Ziwa hasa Mkoa wa Kagera zikieleza kuwa kitu kinachodhaniwa kuwa bomu, kimelipuka katika Shule ya Msingi Kihinga iliyopo kijiji cha Kihinga kilichopo Kata ya Lulenge wilayani Ngara na kusababisha majeruhi.

millardayo.com imempata Mganga wa Hospitali ya Rulenge iliyopo wilayani Ngara, Kagera, Sister Mariagoreth Fransis ambaye amesema wamepokea majeruhi 45 waliotokana na mlipuko huo ambapo kati ya majeruhi hao, 13 wamejeruhiwa vibaya na wawili wamefariki.

millardayo.com inaendelea kufuatilia kwa karibu na itakupa taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo.

Rais Magufuli kaitolea majibu changamoto iliyompigisha magoti Mbunge

Soma na hizi

Tupia Comments